Jiunge nasi

Je wewe ni Mswahili wa Burundi Basi jiunge katika Harakati hizi na ujitoleye.

Ufanye nini ?

Pambana ili kupinga Sheria zinazo bagua waswahili inchini Burundi

Mtazamo wetu

Kabila la Waswahili limekubalika inchini Burundi

Changia:

Kuhamasisha

Kujipanga

Kuteteya

Ilani kwa Waswahili wa Burundi

Leo ni siku mpya inayo anza na kuleta muamko mkubwa kwa jamii ya waswahili wa Burundi na kuanzisha harakati na kasi za kutetea haki za kabila la waswahili. Na ni siku muhimu inakao anzisha msafara wakulikomboa kabila letu zidi ya ubaguzi na zulma ya haki tuanao endeshewa siku baada ya siku.

Toka zama za ukoloni hadi sasa waswahili tunazidi kubaguliwa na kuzulumiwa haki siku baada ya siku na kulikashifu kabila letu na uzalili unao fuatia toka kwenye utawa wabeliji.

Leo tumeamua kusisimama kwa pamoja ilikuipigania na kutetea historia yetu, kabila letu na nafasi yetu katika jamii ya warundi ambao ni jamii yetu na si pia. Tumejikubalisha kuipigania hadhi yetu na kukubaliwa kwa kabila la waswahili sawa sawa na makabila mengine inchini Burundi.

Hakuna mtu anayo haki ya kuwatenga waswahili na hata kuwaita kuwa niwageni katika jamii hii ya warundi. Kwa muda mrefu tulithamini sana na kuwapa uwaminifu mkubwa wafanyasiasa wa Burundi kutoka makabila mengine tukiamini ya kwamba wanaweza ama wana nia ya kujenga jamii ya warundi yenye umoja na haki kwa makabila yote. Lakini historian na vitendo vya wanasiasa wa Burundi vinadhihirisha ubaguzi na chuki kubwa ya wafanyasiasa hao zidi ya waswahili.

Zama za mapambano ya uhuru mwaka wa 1960, vyama vya kisiasa pakiwemo PDC, PP PDR na vingivyo vilizihirisha wazi chuki zao zidi ya waswahili vikidai kuwa waswahili sio warundi kwasabuba wana asili na tamaduni tafauti na makabila mengine.

Na baada ya uhuru chama cha UPRONA kilitutendea unyonge kwa kututenga bila hata kukumbuka juhudi na garama vilivyo fanya na wazee wetu ili mwanamfalme Louis RWAGASORE na chama chake cha UPRONA wa weze kufikia madarakani.

Chama cha UPRONA kilitutenga na kilituzalilisha kwa zaidi ya miaka 30 kama raia wadhalili wasio kuwa na haki wala hadhi katika jamii ya warundi.

Wakati wa mazungumzo ya Arusha tuliweza kuuona uwezo wa wafanyasiasa warundi kutoka makabila mengine wa kukubaliana kulitenga kabila la waswahili katika mkataba wa ubagizi wa Arusha.

Na mpaka sasa historia ya ubaguzi na kutengwa kwa waswahili bado inajirudia katika siasa ya Burundi. Msimamo wa chama cha CNDD-FDD wakuwafurunda waswahili kwenye nyanja za maamuzi ni ushadi kamili wa chuki zidi ya kabila la waswahili inchini Burundi. Chama cha CNDD-FDD na UPRONA ndivyo vyama pekee vilivyo shirikiana na waswahili katika harakati za ukombozi na ambavyo havikusita kuwabagua na kuwazalilisha.

Historia, matukiu na vitendo vya wafanyasiasa kutoka makabila mengine vinatufunza wazi tusitegemei wafanyasiasa ili waswahili tuweze kuipata haki na hadhi yetu katika jamii ya warundi. Msimamo, umoja na harakati zetu ndio njia ya pekee na ya haki yakufikia malengo yetu.

Kikundi chetu si chakisiasa wala cha uasi bali ni kikundi cha wanahakati waswahili watetezi wa haki za waswahili inchini Burundi.

Burundi sio urisi wa makabila ya wahutu na watusi
bali ni Taifa linalo kusanya makabila yote yanayo jenga raia wa Burundi.
sisi waswahili "tunapinga" sheria zote zinazo "wagawiya wahutu na watusi haki zote za raia wa Burundi".
haki sawa kwa wote!

-->

Voulez-vous en savoir plus?

Contactez-nous

Téléphone: + 257 75 852 748

Avenue de l'Amitié numéro 8
Bujumbura-Burundi